Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji Mafinga Steven Shemdoe, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Walimu, Wazazi na Wanafunzi kauli hii ameitoa akiwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Mwinyigumba, iliyopo Halmashauri ya Mji Mafinga kwa Wahitimu wa Kidato cha nne 2025.
Akizungumza katika Mahafali hayo amesisitiza umuhimu wa Wazazi kutoa ushirikiano Mkubwa kwa Watoto wao katika suala la Elimu Na amesema itatutengenezea kizazi Chenye kuleta tija katika Taifa letu na pia kila Mwananchi anajukumu la kumchukulia kila mtoto kama mtoto wake na kumkemea pale anapoona anakosea kwani jukumu la kulea mtoto ni la Jamii nzima.
Kwa Wahitimu wa Kidato cha nne amewapongeza kwa hatua waliofikia na amewaasa ukawe mwanzo mzuri katika Elimu waliyopata wasiishie hapo kwani bado wanahitajika kujiongeza kielimu na pia wajiepushe na tabia mbaya zinazoweza kukatisha ndoto zao za Kielimu.
Pia amewashukuru na kuwapongeza Walimu wote wa shule ya Sekondari Mwinyigumba kwa Elimu na Maadili wanayowapatia Wanafunzi.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.