VIPIGO NA MAJERAHA MENGI KWA WATOTO YANASABABISHWA NA WAKINA MAMA- HUO NI UKATILI WA KIJINSIA.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Queen Sendiga amesema vipigo na majeraha mengi kwa watoto vinatoka kwa akina mama, walezi au wazazi. Tuache huo ni ukatili wa kijinsia.
“Wazazi walezi tumewasogenza pembeni watoto katika jukumu la kuwalea na kuwatunza, ni jukumu letu sote tunatakiwa kuwalinda na kuwakumbatia watoto wetu.”
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo kwa Mkoa wa Iringa Maadhimisho yamefanyika Katika Mji wa Mafinga Shule ya Msingi Makalala.
Amesema kuwa wazazi wengi wamekuwa wakiwatuma watoto katika kutafuta chakula cha familia huku wao wakiwa vilabuni, hii sio sawa kabisa na mzazi atakayekutwa kamtuma mtoto kuuza bidhaa kwaajili ya kulisha familia atachukuliwa hatua kali. Jukumu la watoto ni kusoma, kutunzwa na kupendwa.
“Kuna wazazi wengine wanaenda kwenye shughuli zao na kuacha watoto wakileana nyumbani, unakuta mtoto mdogo wa miaka 10 anawalea wenzake wawili, ni majukumu makubwa tuache wazazi kwani huu pia ni ukatili wa kijinsia.”
Akisoma risala kwa Mgeni rasmi Mtoto Peter Sinkala wa Shule ya Msingi Makalala amesema Watoto wanaomba serikali iwasaidie watoto wote wenye ulemavu tofauti tofauti kupewa vifaa kwaajili ya kusomea na wale watoto wenye uwezo lakini ni walemavu waliofichwa majumbani wapelekwe shule.
Amesema watoto wote ni sawa wa kike na kiume hivyo wasibaguliwe katika kupata haki zao hasa kwenye ngazi za familia, watoto waachwe wasome hasa wa kike ili kuja kutimiza ndoto zao wasikatishwe masomo.
Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali ngazi ya Mkoa, viongozi wa Wilaya ya Mufindi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saad Mtambule, Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer pamoja na wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga.
IMEANDALIWA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO
SIMA BINGILEKI
AFISA HABARI MKUU
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.