Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya MJI Mafinga wakiwa wameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt. Linda Salekwa, Mkurugenzi Bi Fidelica Myovella, Katibu Tawala Ndg. Reuben Chongolo na baadhi ya Wataalamu wamefanya ziara ya Jijini Arusha kujifunza kuhusu :-
-Ukusanyaji wa mapato yatokanayo na Leseni za Biashara
-Uendeshaji wa Maegesho ya malori.
-Uendeshaji wa huduma za usafi.
-Uzoefu katika Utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa kutumia mfumo wa Force Account
-Ukusanyaji wa mapato yatokanayo na chanzo cha Taka na Uzoefu kwenye uendeshaji wa Shule za Msingi za Mchepuo wa kiingereza
Akizungumza Mwenyekiti wa MJI Mafinga Mhe. Regnant Kivinge amesema Halmashauri inatekeleza Miradi Mikubwa ya Kimkakati ya Shule, Masoko na hospitali na Miradi ya TACTIC inayotarajiwa kujenga Stendi ya Kisasa ya Mabasi eneo la Kinyanambo na Ujenzi wa Barabara kadhaa katika MJI wa Mafinga kuanzia mwezi Julai-Agosti 2025.
“Halmashauri ya MJI Mafinga mpaka sasa tunashule moja ya mchepuo wa kingereza ambayo inafanya vizuri sana na tunampango wa kuongeza Shule nyingine ya Mchepuo wa kingereza, tunataka kuboresha ukusanyaji wa Mapato rafiki bila kuwaudhi wananchi wetu lengo likiwa ni kutekeleza Miradi ya Maendeleo na kuongeza mapato
Naye DC- Mufindi Mhe. Dkt. Linda Salekwa amesema Wilaya ya Mufindi inakua kwa kasi kubwa hivyo kuja kujifunza ni mkakati wa kuboresha Ukusanyaji wa Mapato na utoaji huduma bora kwa wananchi.
“ Hakika Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amelenga kuhakikisha sekta zote Zina natoa huduma tarajiwa kwa wananchi Kwani Miradi tunayoona inatekelezwa Arusha, Mufindi na maeneo mengine ya Nchi hakika inagusa maisha ya wananchi.
Waheshimiwa Madiwani wametembelea Ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa AFCON unaojengwa na Serikali ya Tanzania kwa gharama ya shilingi Bilioni 286 na utakuwa na uwezo wa kuchukua watu zaidi I ya 32,000 ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 80.
Ujenzi wa Hospitali ya Nyota tano inayojengwa kwaajili ya kutoa huduma za Afya za kitalii na maeneo ya Shule na Masoko
Waheshimiwa Madiwani Wamepokelewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maximillian Iraqhe ambaye ni Diwani wa kata ya Kaloleni
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Picha mbalimbali za Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu wakiwa katika ziara ya kujifunza mambo mbalimbali katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.