Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya MJI Mafinga ikiongozwa na Mkurugenzi wa MJI Mafinga Bi. FIDELICA MYOVELLA imefanya ziara ya Ufuatiliaji kwenye Mradi wa Umwagiliaji wa Mtula ambao Miradi huu umejengwa na Fedha kiasi cha shilingi Milioni 500 kutoka Serikali Kuu na unahudumia zaidi ya wakulima 200 na Kilimo kinachofanyika katika eneo hilo ni Kilimo cha Mahindi, maharage, vitunguu viazi na nyanya.
Akizungumza Mkurugenzi MJI Mafinga Bi Fidelica Myovella amewashauri wataalamu wa kilimo ngazi ya Kata na Halmashauri kuanzisha shamba darasa katika eneo hilo ili wakulima wengine wajifunze kupitia shamba darasa la Halmashauri ili kuweza kupata mazao bora kwa kufuata kanuni bora za kilimo ikiwamo matumizi za mbolea na faida ya kupima udongo.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.