Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Matilda Yassin amezindua zoezi la kutoa elimu juu afya ya uzazi ya mama na mtoto pamoja na elimu ya lishe katika Kijiji cha Kikombo.
Katika zoezi hilo jumla ya watoto 209 wamepatiwa huduma mbalimbali ikiwemo kupima uzito, kupewa chanjo,dawa za minyoo pamoja na matone ya vitamini A.
Sambamba na hilo Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Water for Afrika wamekabizi kisima kirefu cha maji zahanati ya Kijiji Kikombo ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa na pia wanachi wa maeneo ya karibu wnapata huduma ya maji Safi na salama.
Aidha Bi Matilda amewataka wakina mama kuhakikisha wanahudhuria kliniki ili kujua maendeleo ya mtoto na pia kupatiwa huduma zote ikiwemo chanjo mbalimbali pamoja na kupewa elimu ya uzazi na lishe.
Michael Ngowi Afisa Habari.
Picha mbalimbali katika zoezi la uzinduzi wa utoaji wa elimu ya afya na uzazi pamoja na lishe kitika Kijiji cha Kikombo.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.