Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Mji Mafinga wamepewa Elimu kuhusu Hati fungani ya Samia Miundombinu (SAMIA INFRASTRUCTURE BOND)inayotolewa na Benki ya CRDB. Elimu iliyotolewa na Ndugu Boniface Bunyinyiga Buliga Kaimu Meneja CRDB Mafinga katika Ofisi za Halmashauri zilizopo Luganga.
Amesema dirisha la Hati limefunguliwa na litakuwa kwa kipindi cha Miaka 5 na Hati fungani hizi zipo hatua ya awali mpaka tarehe 17/1/2025 ambapo kufikia tarehe 10/2/2025 Hati fungani hizi zitaanza kununuliwa kupitia Soko la Hisa.
“ Biashara hii haiumizi kichwa tunatamani watanzania waielewe na kununua hisa ambapo unaweza kuwekeza kuanzia 500,000 na gawio lake ni asilimia 12 kwa mwaka lakini inaweza kugawiwa kila baada ya miezi mitatu kulingana na uwekezaji wa mtu, Hati fungani hii maana yake unaikopesha Taasisi na baadae unapata faida”
Lengo la Hati Fungani za Samia ni kusaidia Wakandarasi Wazawa kukabiliana na Changamoto za Kifedha,kuweza kushiriki katika Miradi Mikubwa ya Miundombinu ya Barabara na pia mwekezaji anaweza kupata dhamana ya mkopo kupitia uwekezaji huu wa Hati fungati ya mama Samia.
Imeandaliwa na Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.