Mtihani wa kitaifa wa upimaji wa Darasa la Nne unatarajia kuanza rasmi tarehe 22/10/2025 mpaka 23/10/2025, Kwa Halmashauri ya Mji Mafinga Jumla ya Wavulana 1,864 na Wasichana 1,883 Wanatarajiwa Kufanya Mtihani wa upimaji kitaifa wa Darasa la nne.
Akizungumza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovela amewatakia kila la kheri kwenye Mtihani zaidi ya yote wamtangulize Mungu na wazingatie yale yote waliyofundishwa ili waweze kufaulu vizuri kwenye Mitihani yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi na Awali Bi, Dorothy Kobelo amesema jumla ya Shule 46 za Msingi zinatarajia kufanya mtihani huo wa upimaji ambapo 32 za Serikali na 14 ni Shule binafsi na Wanafunzi 3,277 watafanya mtihani kwa kutumia Kiswahili na 471 kwa lugha ya Kiingereza pia amesema Wanafunzi wenye mahitaji maalum watafanya mtihani wa upimaji wa darasa la nne ambapo 04 wenye uoni hafifu na Wanafunzi wasioona 03.

Bi, Kobelo pia ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kuendelea kushirikiana na Walimu kwa karibu kwa kuhakikisha watoto wanapata msaada na utulivu nyumbani ili waweze kufanya vizuri katika Mtihani.
Na,
Anna Mdehwa.
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.