Wananchi wanaojishughulisha na kilimo maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji Katika Kata ya Boma Halmashauri ya Mji Mafinga wamepewa Elimu kuhusu namna ya kutunza vyanzo vya maji na mpango wa Halmashauri wa kupanda miche ya miti ili kulinda vyanzo hivyo.
Akizungumza Mkuu wa Kitengo Cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Ndugu Demitrus Kamtoni amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa na kuhifafhiwa ili kuepuka kukauka kwa vyanzo hivyo ambavyo vitaleta madhara kwa viumbe hai.
“ Tunalima hadi kwenye mkondo wa Maji, hebu tiache mita 60 ndo tuanze shughuli zetu huko.Tusilime hadi kwenye vyanzo vya maji, tutunze kilichopo ili kiweze kutusaidia, mnalima vinyunguni hadi mnachepusha maji sio sawa? Maji yanategemewa na viumbe hai vyote. Tuyatunze”
Ameongeza kuwa Halmashauri ya Mji Mafinga imepanga kugawa miche aina ya mivenji ili ipandwe baada ya mita 60 kandokando ya chanzo cha maji ili kuhifadhi maji, miche hiyo itakabidhiwa kwa wakulima katika maeneo ya mabondeni.
Aidha Ndugu Kamtoni amesema kuwa, miti iliyopandwa karibu na vyanzo vya maji aina ya milingoti na Mipaina itatakiwa kuondolewa kwani inakausha maji na itaondolewa kwa kibali maalum.
Naye Mzee Obeleti Mnyinga baada ya kupokea elimu hiyo amesema wananchi wa Ihongole wapo tayari kutoa ushirikiana kwa Serikali ili kuwabaini wanaolima ndani ya mita 60 ya vyanzo vya maji na wanasubiri miche hiyo ya miti wataipanda na kuhakikisha wanaitunza.
Elimu ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji inaendelea kutolewa na Halmashauri ya Mji Mafinga kupitia Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa mazingira.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.