Wataalamu kutoka Agricultural Transformation Office (ATO) iliyochini ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvivu wametoa mafunzo kwa Watumishi wa Halmashauri ya Mji Mafinga kuhusu Agricultural Master plan 2050 (Mpango Mkuu wa Taifa wa Kilimo 2050) ambao lengo kuu ni kubainisha maeneo muhimu ya kilimo kama Taifa ambayo yamepewa kipaombele.
Akizungumza Jeremia Temi Kaimu Mkurugenzi kutoka ofisi ya Mageuzi ya Kilimo amewataka Watumishi katika budget zao za idara asa ya Kilimo ni vyema wakapanga vitu kulingana na muongozo wa Mageuzi ya Kilimo 2050 kwani kwa kufanya ivyo itasaidia kufikia lengo lililokusudiwa. Pia amesisitiza wataalamu wa Kilimo ni vyema wakawa karibu na wakulima na kuwapa ushauri kulingana na taratibu za Kilimo zinavyotaka Hata hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella amewapongeza wataalamu hao kwa kuja kutoa mafunzo na pia amesisitiza Kilimo Bora ndicho kitakacho tupa Lishe nzuri kwa jamii zetu.
Imetolewa na,
Anna Mdehwa
Wataalamu kutoka Agricultural Transformation Office (ATO) iliyochini ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvivu wakitoa mafunzo kwa Watumishi wa Halmashauri ya Mji Mafinga kuhusu Agricultural Master plan 2050 (Mpango Mkuu wa Taifa wa Kilimo 2050) ambao lengo kuu ni kubainisha maeneo muhimu ya kilimo kama Taifa ambayo yamepewa kipaombele.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.