“Mradi utazingatia usalama wa kimazingira katika jamiii itayozunguka Mradi na pia naomba watu wote tuwe sehemu ya umiliki wa Mradi kwa kuuangalia na kutoa taarifa sehemu husika pindi tutakapoona kitu cha tofauti” Maneno hayo yamesemwa na Mhandisi Emmanuel Manyanga Mratibu Mradi wa TACTI (Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji ya Tanzania kwa kuhusisha ushindani. Kutoka Ofisi ya Raisi Tamisemi ambaye ameongozana na Wataalamu wengine kutoka Tamisemi. akitoa mafunzo juu ya Mradi katika Halmashauri ya Mji Mafinga ambapo ameelezea Mradi umefadhiliwa na Benki ya Dunia na utafaidisha Miji 45 ikiwemo Halmashauri ya Mji Mafinga.
Kwa Mafinga kupitia Mradi wa TACTIC inategemewa kujengwa Soko la kisasa, Barabara pamoja na Stendi ambapo maeneo Mradi utapita na ikatokea ni eneo la mtu basi atalipwa kwa kufuata utaratibu wa kisheria uliopo.
Aidha Afisa Tawala Robert Kilewo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ameshukuru kwa mafunzo hayo na amesema itasaidia kutujengea uelewa wa pamoja na inapotokea tatizo inakuwa rahisi kujua namna ya kutatua.
Pia Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella ameshukuru kwa Mradi na kuhaidi kutoa ushirikiano ili kutekeleza Mradi kwa wakati na kuleta ufanisi.
Mafunzo hayo juu ya Mradi wa TACTIC yameudhuliwa pia na Wataalamu kutoka Mji wa Mafinga.
Imeandaliwa na,
Anna Mdehwa.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.