“Wale wanaosababisha kuwepo kwa Hoja kwa makusudi kwenye Halmashauri yetu ya Mji Mafinga wachukuliwe hatua, kwani Halmashauri imekuwa ikifanya vizuri kwa miaka sita mfululizo na kupata hati safi, hivyo hatutaki doa na katika eneo la ukusanyaji wa mapato, Mafinga Mji imefanya vizuri kwani kiasi cha shilingi Bilioni 5.5 sio haba mmekusanya vizuri, Niwapongeze Waheshimiwa Madiwani na Mkurugenzi Bi, Happiness Laizer na Timu yake kwa kazi nzuri”
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Queen Sendiga kwenye Mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani kupitia hoja za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021 uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mkuu wa Mkoa amesema, Halmashauri lazima ijipange katika kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kuweza kuongeza mapato ya Halmashauri.
Aidhaa katika Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Mheshimiwa Queen Sendiga amesema Halmashauri ihakikishe Miradi ya Maendeleo inatekelewa kwa kasi na kwa ubora unaotakiwa na fedha zilizotengwa kwaajili ya utekelezaji wa Miradi hiyo zote ziende na kuelekezwa huko bila kukosa.
Kuhusiana na zoezi la Sensa ya watu na makazi tarehe 23 Agosti, Mkuu wa Mkoa ameomba uhamasishaji uendelee kutolewa kwa wananchi ili zoezi liende kufanikiwa kwa maendeleo ya Taifa letu.
Ameongeza kuwa |Ukatili umekuwa ni tishio katika Mkoa wa Iringa, Hivyo tuwe wazi kusema kuhusu matukio ya ukatili kwa watoto wetu. Sio sawa wala haimpedezi Mungu kuwafanyia ukatili watoto wadogo, tusaidiane kuwabaini wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto ili sheria zichukue mkondo wake na tuwe na hofu ya Mungu. Viongozi wa dini suala hili lisemwe popote ili kuwalinda watoto wetu dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi yao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saad Mtambule ameipongeza halmashauri ya mafinga mji kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa Ushirikiano ni Mkubwa kwenye Halmashauri na Ushauri wowote unaotolewa kwenda kwa Wataalamu katika sekta mbalimbali unafanyiwa kazi na wataalamu. Hivyo Halmashauri itaendelea kupata Hati safi na Miradi ya maendeleo itatekelezwa kwa ubora unaotakiwa.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer amesema kuwa atahakikisha Hoja zote zilizosalia zitatafutiwa majibu na majibu hayo yatawasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwaajli ya Uhakiki.
Viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa walihudhuria Baraza hilo Akiwemo Muwakilishi wa RAS Mkoa wa Iringa Ndugu Wilfred Muyuyu na Wataalamu wa ukaguzi ngazi ya mkoa, Wataalamu wa Halmashauri pamoja na wananchi wa Mji Mafinga.
Imeandaliwa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano Mafinga Tc
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.