Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga wamepewa Mafunzo ya Ukaguzi wa ndani katika Ofisi za Halmashauri kwa lengo la kupata Elimu ya Kujikagua katika Idara au Vitengo vyao kabla ya Kukaguliwa na Kitengo Cha Ukaguzi wa ndani.
Mkuu wa Kitengo Cha Ukaguzi wa ndani CPA Godson Kapinga Amesema kuwa umuhimu wa kutoa hayo Mafunzo kwa Watumishi wa Halmashauri ni kuimarisha uwezo wa Idara au Kitengo katika kulinda na kudumisha thamani ya Utoaji wa Huduma kwa Jamii pia kusaidia katika kukuza Maadili yanayofaa na Usimamizi bora katika Utendaji wa Kazi.
“Lengo la mafunzo haya ni kuwapa Elimu ili mpate uelewa ambao utawasaidia Kujikagua ipasavyo katika Idara na Vitengo vyote vya Halmashauri ili kujua Ubora na Upungufu kabla ya Ukaguzi wa ndani haujawafikia,pia Wakaguzi wa ndani kabla ya kufanya Ukaguzi lazima Wazingatie Mpango mkakati na Sheria zitakazowaongoza katika kufanya Ukaguzi.” Amesema.

Pamoja na hayo Afisa Ukaguzi wa ndani Ndugu Robert Kwayu amesema kuwa Idara na Vitengo vyote vya Halmashauri ni Wakaguzi kwa jinsi Wanavyofuata Miongozo na Sheria za Kazi ndivyo Wanasaidia Ukaguzi wa ndani pia Kazi zifanyike kwa Ubora na Utoaji wa Taarifa uwe wa Kuaminika.
Ukaguzi wa ndani ni shughuli huru yenye lengo maalumu la kutoa Uhakiki na Ushauri unaolenga kuongeza Tija na Kuboresha Utendaji katika Halmashauri kwa kuzingatia Usimamizi na Kuimarisha Uthibiti wa ndani na Utawala Bora.
Vedasto Faustine Malima
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.