Akizungumza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Mafinga Dr. Bonaventura Chitopela amewataka kuzingatia kanuni na taratibu za kujikinga na ugonjwa hatari wa Mpox kwani asilimia 11 ya wanaopata wanaweza kufariki kwa ugonjwa huo. Amewataka kuzingatia kutokwenda kwenye mikusanyiko isiyo ya lazima na kunawa na maji tiririka mara kwa mara au kutumia vifaa vya kusafishia mikono.
Aidha Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji Mafinga Gaudence Haule amewataka wazingatie kanuni za kujilinda na ikitokea kuna mtu anadalili zozote za ugonjwa watoe taarifa mapema kwa mamlaka zinazohusika ili mtu apatiwe matibabu na kuzuia ugonjwa kuweza kuzidi kuenea katika jamii yetu.
Pia Charles Mwaitege Afisa Utumishi ameshukuru wataalamu wa Afya wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kutoa elimu kwa Watumishi “Niwashukuru kwa kutoa elimu hii kwani tumepata uelewa mzuri kuhusu huu ugonjwa na uhakika kila mtu atakuwa Mwalimu mzuri kwa familia yake na jamii inayomzunguka” Amesema Charles Mwaitege.
Kwa upande wake Dorothy Kobelo Kaimu Mkurugenzi alifunga kikao hicho cha kuwajengea uwezo Watumishi wa Mji Mafinga dhidi ya kujikinga na ugonjwa wa Mpox kwa kuwasihii Watumishi kuzingatia yale waliyofundishwa.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.