WAZAZI WAIOMBA SERIKALI KUJENGA SHULE NYINGINE YA MCHEPUO WA KINGEREZA (ENGLISH MEDIUM )KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA.
“Tunaiomba Serikali ijenge Shule nyingine ya Mchepuo wa Kingereza kama hii ya Chief Mkwawa English Medium kwa wazazi wanaotamani kusomesha watoto wao shule kama hizi kwani imekuwa ni Shule ya mfano kwa Shule za Mchepuo wa Kingereza ufaulu ni mzuri, Ada yake unaweza kulipa kwa Awamu, watoto wanakula chakula bora, Usafiri wa kutosha na walimu wenye ujuzi wa kutosha . Tunamshukuru sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathanini watoto wetu kwa kuwaletea elimu bora. Tunaiomba Serikali ijenge shule nyingine maana hii tayari imeanza kujaa na wazazi wanaikimbilia kwakuwa ufundishaji na elimu inayotolewa na huduma hakika sisi wazazi tunarizika”
Kauli hiyo imetolewa na Mzazi Bi, Tumaini Kikumbwe alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari hizi alipotembelea na kujionea mafanikio makubwa katika Shule hiyo ya Kingereza inayomilikiwa na Serikali chini ya Uongozi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Chief Mkwawa English Medium ni Shule ya Serikali ya Mchepuo wa Kingereza inayomilikiwa na Halmashauri ya Mji Mafinga
Shule imesajiliwa rasmimwaka 2023 kwa usajili wa namba EM 20111 nakuanza kudahili wa wanafunzi tarehe 12 Januari 2024. Shule ina jumla ya wanafunzi 225.
Na
Sima BINGILEKI
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.