Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe,DK Linda Salekwa akifungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Vijiji,Mitaa na Vitongoji wa Halmashauri ya Mji Mafinga wenye lengo la kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Leo 15/01/2025 ambapo amewataka kufanya kazi kwa Weledi na kufuata Sheria za Nchi kwani hakuna ambaye Yuko juu ya Sheria na pia amewataka kuhakikisha kila Mtoto aliyefikisha umri wa Kuanza shule katika maeneo Yao wahakikishe Wazazi wanawapeleka Shule kwani Elimu bure hivyo hakuna kisingizio chochote .
“Naomba mkafanye kazi kwa kushirikisha Wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa walizonazo hata kama ni tofauti na yako.” Amesema Mhe,Dkt Linda Salekwa
Aidha Mafunzo haya yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Mji Mafinga na Kushirikiana na Wataalamu kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo Mhadhiri Boniface Kumburu kutoka Chuo icho amewasisitiza katika mada ya Uongozi na Utawala Bora kama Viongozi wanatakiwa kuonyesha njia ya mafanikio katika kutatua matatizo katika eneo husika na pia amewataka kukataa Rushwa kwa maneno na matendo.
Pia Jonas Kapwani Mhadhiri Kutoka Chuo cha Hombolo amewataka wasiwe sababu za migogoro kwenye maeneo yao kwani lengo la Serikali ni Ustawi wa Wananchi na amewakumbusha Madaraka waliyonayo wamepata kwa Wananchi ndio mana wakapigiwa Kura hivyo ni muhimu kuwa chanzo cha Amani na Mshikamano kwenye maeneo yao.
Mbali na hayo wamejifunza kuhusu Usimamizi wa Ardhi na mipaka yao katika utendaji.
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.