Wilaya ya Mufindi kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 Halmashauri zake zimefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Bilioni 13.3”
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt.Linda Salekwa @salekwalinda akiwasilisha taarifa ya Utekelezaju wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Januari- Disemba 2024 kwenye Mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi.
Amesema Halmashauri ya Mji wa Mafinga ilikusanya jumla ya Shilingi Bilioni 6.2 na Halmashauri ya Wilaya Mufindi ilikusanya Bilioni 7.1 B sawa na asilimia 96.5 ya jumla , Halmashauri ya Mji Mafinga asilimia 113 na Wilaya Mufindi asilimia 85.5 na kufanya jumla ya mapato kusanywa kuwa Bilioni 13.3
Aidha Makusanyo ya mapato ya Ndani kipindi cha Julai hadi Disemba 2024 Halmashauri ya Mji Mafinga imeweza kukusanya Bilioni 2.9 Sawa na asilimia 44 na Wilaya Mufindi Bilioni 3.4 sawa na asilimia 38.6
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi Mh.George Kavenuke amesema Wilaya ya Mufindi imekuwa ikifanya vizuri kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Barabara pamoja na Ukusanyaji wa mapato hivyo kuwahimiza Wataalamu kuendelea kusimamia Miradi ya Maendeleo kwa ufanisi ili Miradi yote inayoletwa ikamilike kwa wakati kama ambavyo Serikali imekusudia.
“ Tunamshukuru Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta Fedha nyingi za Utekelezajii wa Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Mufindi, tuna Mradi mkubwa wa MAUWASA Kupitia Serikali Kuu ambao imetengewa jumla ya Shilingi Bilioni 49.5 kwaajili ya Usanifu Ujenzi na usimamizi wa Mradi wa maji katika Mji wa Mafinga pamoja na Miradi mingine, haya ni mafanikio makubwa.”
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kimehudhuriwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu kutoka kwenye Kata 36 Wakurugenzi wa Halmashauri, Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, DAS na Wajumbe.
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga TC
Wajumbe wakifatilia Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambacho kimehudhuriwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu kutoka kwenye Kata 36 Wakurugenzi wa Halmashauri, Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, DAS na Wajumbe.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.