WILAYA YA MUFINDI YAVUKA LENGO UKUSANYAJI WA MAPATO-DC MUFINDI DKT.LINDA SALEKWA
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amewasilisha kwa taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Januari-Juni 2023 katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Mufindi, taarifa inayojumuisha Halmashauri ya Mji Mafinga, Halmashauri ya Mufindi na Taarifa za RUWASA, TANESCO na TARURA.
Amesema Wilaya ya Mufindi imepiga hatua katika Sekta mbalimbali kutokana na Juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuleta Mabilioni ya fedha wilayani humo na wataalamu kuhakikisha fedha hizo zinafanya lengo lililo kusudiwa.
Dkt. Salekwa amesema katika Ibara ya 122 kuhusu ukusanyaji wa mapato Wilaya ya Mufindi imevuka lengo la Ukusanyaji kwa kukusanya zaidi ya asilimia 100. ambapo Kwa Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2023 imekusanya jumla ya shilingi 5,747,829,634.48 sawa na asilimia 102 ya Lengo. Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imekusanya 5,670,414,489,000/- na kufanya makusanyo yote jumla kuwa 11,418,244,123,000/- sawa na asilimia 91.21 ya makadirio.
Katika Ibara ya 86 Lishe, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amesema asilimia ya watoto chini ya miaka 5 wenye ukondefu imepungua kutoka 1.9 hadi 0.7 mwezi Juni , 2023 na kiwango cha unyonyeshaji wa maziwa ya mama kutoka asilimia 93 hadi kufikia asilimia 98.8 mwezi Juni 2023. Aidha idadi ya wataalamu wa afya waliojengewa uwezo wa kutoa huduma za lishe imeongezeka kutoka wataalamu 217 hadi kufikia wataalamu 227 katika Wilaya ya Mufindi.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa George Kavenuke amepongeza Mkuu wa Wilaya na Wataalamu kwa taarifa nzuri yenye kubeba kila sekta na kuwashukuru Waheshimiwa Madiwani kwa usimamizi mzuri wa Miradi ya Maendeleo na zaidi kutoa Shukrani kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta Mabilioni ya Fedha katika Wilaya ya Mufindi.
“ Ili kumuonyesha Rais kwamba tunathamini Fedha tunazoletewa kwaajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo lazima tuzisemee tusikae kimya yanayofanywa ni makubwa mno tutangaze Miradi na wananchi wajue kazi nzuri inayofanywa na Mheshimiwa Rais”Ufaulu umeongezeka wa darasa la saba kufikia asilimia 96.6 na wilaya ina jumla ya madarasa ya shule za Msingi 1717.” Hii ni hatua kubwa huku tukiendelea kukusanya mapato ya Serikali”
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.