Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Serikali yake ya Awamu ya Sita imetujengea Miundombinu Mizuri ya Madarasa na kutuletea vifaa vya kujifunzia kama leo tumepokea Kompyuta 8, ( LENOVO) kompyuta mpakato moja na Projekta 1 kutoka Wizara ya Elimu chini ya mpango wa SEQUIP, yote haya hayatakuwa na maana kama wanafunzi watakuwa hawahudhurii masomo na wanafeli. Tushirikiane wazazi na Walimu kuhakikisha maendeleo ya wanafunzi wetu yanakuwa mazuri na ufaulu unaongezeka”
Kauli hiyo imetolewa na Mheshimiwa Denis Kutemile Diwani wa Kata ya Saohill alipokuwa akizungumza na wazazi kwenye mapokezi ya vifaa vya Tehama kutoka Wizara ya Elimu kwenye Mpango wa SEQUIP.
Amesema Vifaa hivyo vitasaidia kuongeza Ufaulu kwa wanafunzi kwani mitihani itachapishwa hapo na kurahisisha mikutano na kuongea ujuzi kwa wanafunzi katika sekta ya Tehama.
Naye Bi. Daines Msola Diwani wa viti maalumu na Mlezi wa Kata ya Saohill amesema ili watoto wafaulu inahitaji ushirikiano na malezi ya Wazazi na Walimu, bila ushirikiano na kuwafuatilia watoto kuwapekua, kukagua madaftari yao wanapotoka shule ni kumpoteza mtoto kwani bila kufuatiliwa ufaulu wao unafifia.
“ Wazazi niwaambie , kutochangia Chakula cha wanafunzi mashuleni na kutowapa mavazi kama vile Uniform huo ni Ukatili, Nawaomba wazazi na walimu tutimize wajibu wetu na tusimame kwenye nafasi zetu kama wazazi”
Akizungumza Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji Mafinga Mwalimu Stephen Shemdoe amesema ufuatiliaji wa Chakula cha mchana kwa wanafunzi na mahudhurio ya wanafunzi vitakuwa dhamani yake lengo likiwa ni kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo unaongezeka.
“Tujiulize kwanini wanafunzi wanafeli, tatizo liko wapi? Wazazi tunawaachia walimu kufundisha wanafunzi na kuwalea hii sio sawa, lazima tufuatilie maendeleo ya wanafunzi wetu mashuleni”
Shule ya Sekondari Saohill yenye wanafunzi 273 imejengwa na fedha kutoka Serikali Kuu kiasi cha Shilingi Milioni 470 kwa mpango wa SEQUIP
Imeandaliwa na
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.