Kamati ya Ulinzi na Usalama (W) Mufindi tarehe 30/3/2023 imepitia Miradi pendekezwa itakayo Zinduliwa, Kaguliwa, Pitiwa na Kuwekewa Jiwe la Msingi na Mwenge wa Uhuru 2023 ambao unatarajiwa kukimbizwa Halmashauri ya Mji Mafinga Tarehe 3/5/2023 .
Mwenge wa Uhuru Unatarajiwa kukesha katika Uwanja wa Mshujaa na tarehe 4/5/2023 Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa wilaya ya Kilolo.
Akizungumza kuhusu Miradi pendekezwa itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023, Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Henry Kapela ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Michezo Utamaduni na Burudani amesema kuwa Mwenge unatarajiwa kupokewa tarehe 3/5/2023 na utapitia Miradi pendekezwa ifuatayo:-
-Kuweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Lush
-Kuzindua kitalu cha Miche-Pandamiti
-Kuzindua Maabara Uoendo Sekondari
-Kuweka Jiwe la Msingi Chief Mkwawa English Medium
-Kuzindua Kituo cha Mafuta NFS
-Kuzindua EMD jengo la kutoa huduma kwa wagonjwa wa dharura- Hospitali ya Mji
-Kukagua vikundi vilivyopokea mikopo Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu.
Kapella amesema Mwenge wa Uhuru unatarajiwa Kukesha katika Uwanja wa Mashujaa Mjini Mafinga na Tarehe 4/5/2023 utakabidhiwa Wilaya ya Kilolo.
Ziara hiyo pia imehudhuriwa na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Mafinga ikiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer na waratibu wasaidizi wa Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Mji Mafinga 2023.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.