Mkurugenzi Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella akiwa ameongozana na Wakuu wa Idara wamefanya ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo lengo likiwa ni kushauri na kusukuma ukamilishaji wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika ngazi ya Kata.
Amesema katika Ukamilishaji wa Miradi lazima vipaumbele vizingatiwe ili Mradi ukamilike na uweze kutumika.
Suala la manunuzi lifuatiliwe kwa ukaribu ili manunuzi yafanyike na jengo likamilike kwa wakati na liweze kuanza kutumika kwa muda uliopangwa .

Aidha Timu ya Menejimenti imetembelea Kituo cha Afya Bumilayinga ambapo kuna ukamilishaji wa Jengo la kuhifadhia Miili na ukamilishaji wa kumalizia chumba cha upasuaji ambapo Halmashauri imetoa kiasi cha shilingi
Milioni 23.4.

Aidha Timu ya Menejimenti imetembelea Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi ya JJ Mungai itakayokuwa na Mkondo Mmoja na yanajengwa Madarasa 2 ya Awali na Matundu 6 ya vyoo kwa Wavulana na Matundu 3 na Wasichana Matundu 3 pia Yanajengwa Madarasa 6 ya Wanafunzi ambayo yatakuwa na Matundu ya Vyoo 10 kwa Wavulana Matundu 5 na Wasichana Matundu 5.Fedha zinazotumika katika Ujenzi wa Shule ya JJ.Mungai ni Shilingi Milioni 326,500,000 kutoka Serikali Kuu kupitia Mpango ws BOOST ambapo ujenzi upo katika hatua ya kuezeka.

Aidha Mkurugenzi amesema kuwa fedha zilizopokelewa kwaajili ya PROGRAMU YA BOOST( Awamu ya Tatu)
ni kwaajili ya Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi JJ MUNGAI 326,500,000 /-na
Shule ya Msingi Lumwago imepokea Kiasi cha Shilingi 112,000,000 /- kwaajili ya Ujenzi wa Madarasa 4 na matundu 6 ya vyoo pamoja na mapokezi ya shilingi Milioni 69.1 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 2 ya mfano ya Awali na matundu 6 ya vyoo.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga Tc
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.